Ligi

Nisipowafunga SIMBA kachomeni nyumba zangu moto-Mrisho Ngassa

Sambaza....

Homa ya pambano la jadi kati ya Simba na Yanga inazidi kupanda kila uchwao. Hii ni mechi ambayo hushika hisia za Watanzania wengi. Ni mechi ambayo husimamisha nchi.

Asilimia kubwa ya mashabiki wa mpira wa miguu Tanzania ni mashabiki wa Simba na Yanga ndiyo maana inaonekana mechi hii kuwa na hisia kubwa sana.

Mashabiki wa Simba wakiwakebehi Yanga

Kuelekea mechi hii ya tarehe 04/01/2020, tujikumbushe ahadi moja ambayo uliwahi kutolewa na mchezaji mahiri wa Yanga , Mrisho Ngassa.

Mrisho Ngassa mwaka 2013 tarehe 20 October aliweka ahadi ya nyumba zake kuchomwa moto kama asipofanikiwa kuifunga Simba kwenye mechi hiyo iliyochezwa tarehe 20/10/2013 kwenye uwanja wa Taifa.

Aliyekuwa kocha wa Simba kwa wakati huo Abdallah Kibadeni alimbeza Mrisho Ngassa , mashabiki wa Simba wengi walimbeza Ngassa Mrisho na walimpania sana.

Lakini mwisho wa Siku alikuwa mtu wa kwanza kufunga goli kwenye mechi hiyo, mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya magoli 3-3, Yanga walienda mapumziko wakiwa wanaongoza magoli 3 lakini kipindi cha pili walisawazishiwa.

Swali la kujiuliza Mrisho Ngassa anaweza kutoa tena ahadi kama hii kuelekea mechi ya watani wa jadi ya tarehe 04/01/2020?


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.