Sambaza....

Kuelekea katika mchezo dhidi ya KMC kuliripotiwa kuwa Ibrahim Ajib anaumwa na asingeweza kucheza katika mchezo huo. Kwa habari za ndani ya klabu ya Yanga , Ibrahim Ajib yupo katika mgomo baada ya kutolipwa mshahara wa miezi miwili.

Hali inaonekana ni tête katika klabu ya Yanga na imepelekea baadhi ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho cha Yanga kuanzisha mgomo baada ya kucheleweshwa mshahara wao wa miezi miwili. Golikipa namba moja wa klabu hiyo , Beno Kakolanya pia ameingia kwenye mgomo huo akishikiza madai yake. Kwa habari za ndani ambazo Kandanda.co.tz imezipata , Beno Kakolanya naye yupo kwenye mgomo huo.

Hii siyo Mara ya kwanza kwa wachezaji wa Yanga kugomea kushikiza madai yao, msimu jana pia waligoma katika vipindi tofauti baada ya klabu hiyo kupitia wakati mgumu wa ukata.

Sambaza....