Tetesi

Norwich yambakiza kidogo Samatta

Sambaza....

Watanzania wengi wamekuwa na hamu ya kumuona Mbwana Samatta akiwa kwenye ligi ya England ligi ambayo inafuatliwa na watu wengi duniani. Na ndiyo ligi pendwa hapa nyumbani Tanzania.

Norwich wanaonekana kuhitaji huduma ya Mtanzania huyo anayekipiga KR Genk kwa sasa . Norwich imeshapeleka ofa mbalimbali kwenye timu ya KR Genk kwa ajili ya kumsajili Diego Captain Mbwana Samatta.

Mara ya kwanza Norwich walitoa ofa ya Euro 10M lakini Leo hii wameongeza ofa na wametoa Euro 11 kwa ajili ya kumsajili Mbwana Samatta.

Endapo Mbwana Samatta “Diego Captain” atasajiliwa atakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya England kama alivyokuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.