Tetesi

Novatus Dismas Kutimkia Uingereza

Sambaza....

Kulingana na Daily Mail, Southampton na Middlesbrough wana nia ya kumsajili Novatus Miroshi wa Zulte Waregem. Mtanzania huyo mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na timu hiyo msimu uliopita wa kiangazi akitokea Israel, lakini ameendelea kushangaza kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi.

Mpaka sasa msimu huu, Miroshi amecheza kama kiungo wa kati, beki wa kushoto na kama mlinzi wa kati katika mfumo wa mabeki watatu nyuma. Licha ya kushuka daraja kutoka Pro League, haishangazi kuona nyota  huyo wa Kitanzania akionekana kuvutia vilabu vya nje ya Ubelgiji.

Miroshi alicheza mechi 36 kwa Zulte Waregem msimu huu. Alishindwa kufunga lakini alitoa pasi mbili za mabao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 pia ameichezea timu ya taifa ya Tanzania akiifungia Taifa Stars mabao mawili.

Novatus Dismas.

Nyota huyo wa zamani wa Azam Fc na Biashara Unites amekua na muendelezo mzuri tangu atimke nchini na kwenda nje ya nchi kutokana na kiwango chake anachokionyesha katika vilabu vyote alivyopita tangu Israel na sasa Ubelgiji.

Baada ya kuondoka Azam Fc Novatus alijiunga na Makabi Tel Aviv ya vijana kabla ya kufanya vyema na kupandishwa timu kubwa na katika msimu wa 2022/2023 alijiunga na Zulte Waregen ambayo yupo mpaka sasa ya nchini Ubelgiji. 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.