Sambaza....

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) Emmanuel Amunike amewaondoa kikosini wachezaji sita wa timu ya soka ya  Simba ya jijini Dar es Salaam isipokuwa golikipa Aishi Manula wakidaiwa kutoripoti kambini kwa wakati, na ameteua wachezaji wengine kuziba nafasi zao.

Wachezaji walioondolewa ni pamoja na Nahodha msaidizi John Bocco, Shiza Kichuya, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude pamoja na Hassan Dilunga.

Badala yake, amewachukua mabeki, Ally Sonso, Paul Ngalema wa Lipuli FC ya Iringa, Salum Kimenya wa Tanzania Prisons ya Mbeya, David Mwantika, viungo Frank Domayo wa Azam FC, Salum Kihimbwa na mshambuliaji Kelvin Sabato, wote wa Mtibwa Sugar.

Awali wachezaji hao hawakuwepo kwenye kikosi cha wachezaji 25 ambacho kilitajwa Agosti 21 mwaka huu kujiandaa na mchezo wa Kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika dhidi ya Uganda Septemba 08, 2018.

Sambaza....