Ligi

Okwi wa nini ?, tunaye Deo Kanda

Sambaza....

Ligi kuu Tanzania bara imeendelea tena Leo kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam ambapo Simba ilikuwa inaikaribisha Ndanda FC na Simba ikafanikiwa kushinda magoli 2-0.

Magoli ya Simba yalifungwa na Francis Kahata aliyefunga kwa mpira wa adhabu karibu kabisa na eneo la hatari. Kipindi cha pili Simba waliongeza goli la pili kupitia Deo Kanda aliyetokea Benchi.

Baada ya mchezo huo mashabiki wengi wa  Simba waliohudhuria mechi hiyo walisikika wakidai kwa sasa hawakumkumbuki tena Emmanuel Okwi kwa sababu wana Deo Kanda.

“Hatuna shida na Emmanuel Okwi tumeshamsahau kwa sasa kwa sababu tunaye Deo Kanda ambaye kaziba nafasi yake vizuri”-alisikika shabiki mmoja. Deo Kanda mpaka sasa amefunga magoli 2 katika mechi 3 zilizopita za ligi kuu msimu huu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.