EPL

Ole: United inahitaji alama 15 kuingia ‘Top Four’!

Sambaza....

Meneja wa klabu ya soka ya Manchester United Ole Gunnar Solskajaer amesema ili waweze kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye ligi kuu England ni lazima washinde michezo mitano kati ya sita ambayo imebaki.

Ole ameyasema hayo baada ya timu yake kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Wolverhampton Wanderers jana kwenye uwanja wa Molineux na kufanya matumaini ya kuingia kwenye timu nne bora kuanza kufifia tena.

“Tulikuwa tunahitaji alama 15 kutoka kwenye michezo saba, sasa tumebakiwa na michezo ita pekee, hatuna nafasi tena kwa ajili ya kupoteza mchezo wowote, ni ngumu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali, lakini sisi ni timu nzuri, hivyo itakuwa ngumu zaidi kwa timu ambayo itacheza na sisi,” amesema

Baada ya kichapo cha jana United wameendelea kusalia katika nafasi ya tano huku wakiwa na mchezo mmoja mbele ya timu zote kutoka London ambazo ndizo wanapambana kuwania nafasi mbili zilizobaki kukamilisha zile nne ambazo zitaiwakilisha England kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Na ikumbukwe kwamba Manchester United wamebakiza kucheza na Westa Ham United, Everton, Manchester City, Chelsea, walioshuka daraja Huddersfield Town na watamaliza nyumbani dhidi ya Cardiff City.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x