Sambaza....

Mbona hutuambii kama umeshamuona Pacom Zouzoua? Mbona uko kimya? Wewe utakuwa Simba Sc. Ndio nimemuona Pacome.

Kiufupi tu, jamaa ni fundi wa mpira. Anavutia kumtazama. Kila mara unatamani apewe mpira yeye ili ukwangalie.

 

Ndio, juu ya ufundi wote alionao hapaswi kulinganishwa na Clatous Chota Chama. Ni mapema mno kufanya hivyo kwa sasa.

Katika ligi yetu “Mwamba wa Lusaka” Chama ameshashinda kila kitu. Ni kumuonea Pacome kumfananisha na mchezaji aina ya Chama, Pacome aliyejiunga Yanga Sc miezi miwili iliyopita. Kitafika kipindi cha kuwafananisha, lakini sio sasa.

Pacome Zouzoua akifanya yake uwanjani.

Anachokifanya Pacome leo Chama amekifanya miaka mitatu iliyopita na anaendelea kufanya katika mpira wetu. Pacome aachwe acheze mpira, asifananishwe na Chama. Nadhani Case Closed.

Sambaza....