Mashindano

Pape Sakho ameshinda tuzo kwa mengi, si tu goli zuri!

Sambaza....

Wapwa, nianze kwa kumpongeza mshindi Pape Sakho kwa kutwaa tuzo hii ya goli bora la mwaka CAF. Si vibaya pia nikiipongeza na klabu yake anayoichezea Simba sc na mashabiki wake wote.

Pongezi zaidi kwa muhusika zinatokana na maandiko kadha niliyoyafanya kuelekea tuzo hizo ikiwa ni sehemu ya tafiti zangu binafsi nakumbuka siku ya kwanza washindani wametajwa nikasema kama Mtanzania natamani kuona Sakho anashinda kwa kuwa siku ya tuzo piga garagaza ua jina la Tanzania litatajwa, kutajwa kwake kutangaza Simba na Ligi yetu kiujumla.

Pape Osmane Sakho.

Matumaini yangu hili limefanyika, tafiti ya pili niliandika kuhusiana na nguvu ya mitandao ya kijamii za vilabu kwenye maeneo kama haya ambayo kura inapingwa na yeyote.

Wapwa zangu nikuambie siri ambayo yawezekana hukupata kuifahamu Sakho aliingia ukumbini tayari akiwa mshindi. Kuwa na wafuasi wengi wa mitandao ya kijamii ambao akiamua na kuhamasishwa na kupiga kura lazima utashinda kwa kuwa nafasi ya kuchagua mshindi ilikuwa wazi kwa yeyote.

Ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba Sc.

Simba kwenye ukurasa wake rasmi ya Instagram ina wafuasi 3M, Gabadinho Mhango (kabla hajahama) na Orlando Pirates yake wana 568k, Zouhair El Mutarajia pale Wydad wana 1.1M hapa ni ushindi tayari.

Hata ukiangalia kurasa zao binafsi Sakho licha ya kuwa na 140k wengine wapo chini ya 100k hii inaonesha jinsi gani alivyokuwa na nguvu zaidi yeye ya kushinda.

Kwa hili linakwenda kuthibitishwa na kura zao kwa mujibu wa CAF hadi siku moja kabla zoezi kufungwa Sakho alikuwa anaongoza kwa 71.4% huku anayemfuatia kwa mbali ni El Mutarajia 17.6% na Gabadinho 11% toka kwenye kura 9600+

Mashabiki wa klabu ya Simba.

Ukiangalia ukurasa rasmi wa Instagram ya CAF wakiwa wameweka washindani na katika kinyang’anyiro hiki mashabiki wa Simba walikuwa wanaweka maoni kwa wingi kwamba goli la Sakho ni bora maana yake
kurasa ile ilikuwa inakusanya maoni pia.

Katika maoni 3600+ zaidi 2700 ambayo ni 90% zilikuwa zinamtaja Sakho kama mchezaji anayestahili hivyo kama tungepata mshindi mwingine manung’uniko yangekuwa mengi mno.

Pape Osmane Sakho akikabidhiwa zawadi yake na mchezaji wa zamani wa Nigeria Jay Jay Okocha.

Nikirejea aina ya goli la “Acrobatic” nilishawahi kulizungumza kwenye aina ya tuzo za Puskas sina mashaka hata kidogo.

Na kwa maana moja au nyingine pia unaweza kukubali hata lile goli bora (la Fiston Mayele) la msimu kwenye NBC premier league lilistahili.

Sambaza....