Shirikisho Afrika

Rais Yanga: Mashabiki wa Yanga Wanataka Ushindi

Sambaza....

Baada ya kurejea kutoka nchini Algeria Rais wa klabu ya Yanga amesema anajua mashabiki wa Yanga wamewaamini viongozi na wanataka matokeo mazuri na mafanikio kwa klabu yao ya Yanga.

Msafara wa Yanga umerudi usiku huu  wakitokea Algeria katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Algier ambapo walipata ushindi wa bao moja bila lakini haukutosha kuipa Yanga ubingwa wa michuano hiyo.

Akizingumza na tovuti ya Kandanda.co.tz akiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere baada ya kutua kutoka Algeria Rais wa klabu ya Yanga amesema ” Mashabiki na wanachama wa Yanga wanataka mafanikio na tupo hapa kwaajili hiyo, wametuamini na ndio kitu tunakifanya,” aliongeza Mhandisi Hersi  “Tutahakikisha tunaweka juhudi sana katika kuleta ushindi kwa timu yetu.”

Denis Nkane na Kibwana Shomari wakiwa na medali zao za mshindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika

Rais wa Yanga pia hakusita kushukuru na kuwapa hongera wachezaji pamoja na benchi la ufundi huku pia akijivunia medali waliyoipata katika michuano hiyo.

“Tumerudi hapa tukiwa na matokeo ambayo wengi walikua hawayatarajii na wengine walikua na imani nasisi wakijua tutapata matokeo lakini hayakutosha kuchukua ubingwa.

Kikubwa tunamshukuru Mungu tumerudi na medali za mshindi wa pili za Caf Confederation ni jambo kubwa ni jambo ambalo tuajipongeza, tunawapongeza wachezaji wetu pamoja na benchi la ufundi na mashabiki wetu.” 

Sambaza....