Kocha wa klabu ya Simba Robertinho Oliveira
ASFC

Robertinho Awasifu Wachezaji Wake, Arudi kwa Mashabiki

Sambaza....

Baada ya ushindi wa kishindo walioupata Wekundu wa Msimbazi Simba mbele ya Ihefu na kuwavusha mpaka nusu fainali kocha wa klabu hiyo Robert Oliveira ameonekana kufurahishwa na kiwango cha wachezaji wake.

Kocha huyo Mbrazil alisema walicheza vizuri na ndio maana waliibuka na ushindi wa mabao matano kwa moja na aliwatoa wachezaji wake muhimu kipindi cha pili ili kutunza nguvu zao kwani wana ratiba ngumu mbele yao.

 

Robert Oliveira “Tumecheza vizuri, tumepata mabao mengi na tumeingia nusu fainali hilo ni jambo zuri. Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi nzuri waliyofanya” alisema na kuongeza

“Baada ya kupata mabao manne kipindi cha kwanza ilibidi niwapumzishe baadhi ya wachezaji na kuwaingiza vijana sababu tuna ratiba ngumu iliyo mbele yetu,” amesema Robertinho Oliveira.

Kwa upande mwingine Robertinho amewashukuru mashabiki wa Simba waliojitokeza kwa wingi katika Dimba la Azam Complex  kuwapa sapoti wachezaji wao na mara zote wamekuwa wakifanya hivyo.

“Nawashukuru mashabiki kwa kuja kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu, wanachangia kiasi kikubwa matokeo yanayopatikana uwanjani,” alisema Robertinho.

Baada ya ushindi huo sasa Mnyama Simba atakutana na Azam Fc katika nusu fainali ya michuano hiyo ya FA. Msimu uliopita Simba waliishia nusu fainali kwa kufungwa na Yanga ambao ndio walitwaa ubingwa huo.

Sambaza....