BlogLigi Kuu

Ruvu Shooting: Tumepokea salamu za Matola, ila………..

Sambaza....

Klabu ya soka ya Ruvu Shooting imeitahadharisha timu ya soka ya Lipuli FC kuwa wasitarajie mteremko katika mchezo wao unaofuata wa Ligi kama iivyokuwa kwa Biashara United kwa kupata ushindi wa mabao 3-1.

Ruvu Shooting kupitia kwa Msemaji wao Masau Bwire imesema kwamba imepata ujumbe kutoka kwa kocha msaidizi Seleman Matola wa Lipuli akisema kipigo walichotoa kwa Biashara watakitoa na kwao lakini kama timu wameshajipanga kuhakikisha wanatoa kichapo ili iwe fundisho.

Masau amesema wao watauchukulia mchezo huo ambao utafanyika Disemba 10 kama mazoezi tu kwa ajili ya mchezo utakaofuata dhidi Mabingwa wa kihistoria Yanga SC.

“Lipuli tumewasikia kupitia kwa mwalimu wao Selemani Matola, akitamba kwamba kile ambacho wamekifanya dhidi ya Biashara United wanataka kukithibitisha kupitia sisi, hatuna pingamizi katika hilo kwa sababu wao wamezungumza,”

“Lakini sisi mchezo dhidi ya Lipuli ni maandalizi ya mchezo dhidi ya vinara wa Ligi Yanga, kwa mchezo dhidi ya Lipuli tunataka kuthibitisha nini tunakwenda kukifanya dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Taifa,” amesema.

Masau amesema kikosi chao kinajiandaa kwa sasa kwa ajili ya safari kuelekea Iringa ambapo lengo lao ni kuhakikisha wanathibitisha ubora wao kwa kupata alama tatu katika kila mchezo uliopo mbele yao wakitumia mfumo wa Papasa Square.

“Tunahitaji kuanza safari Disemba 8, mapema kabisa kuelekea Iringa, tutaondoka wachezaji 20 na viongozi Saba, kikosi ambacho maandalizi yake yanaendelea, kilichobaki sasa Hivi ni kufanya tu marekebisho ya Yale ambayo tuliyaona kama mapungufu katika michezo iliyopita,” Masau amesema.

Mchezo uliopita Ruvu Shooting walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuho uliopo Mbweni jijini Dar es Salaam, matokeo ambayo yaliwafanya kufikisha alama 17 na kukalia nafasi ya 12 baada ya michezo 15.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x