Blog

Saa saba ya Simba imejibu!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba mwanzoni mwa wiki hii ilitikisa katika mitandao ya kijamii baada ya kutangaza kurudia kwa mtindo wao wa kutangaza usajili wakati wa saa saba mchana kama ambavyo walikua wakifanya msimu huu mwanzoni. Katika kurasa zao za twitter na instagram waliwataka wapenzi na mashabiki wake wakae mkao wa kula.

Kupitia chaneli yake ya Youtube Mtendaji Mkuu wa klabu na Msemaji wa Simba walikua live leo kuanzia saa saba na kuzungumzia mambo mbalimbali ya klabu ikiwepo usajili, siku ya kuanza mazoezi na uzinduzi wa tovuti ya Simba sc.

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Masingisa akiwa na msemaji wa Simba Hajji Manara.

Siku ya kuanza mazoezi!

Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa msemaji wake Hajji Manara na Mtendaji wake mkuu Senzo Masingisa wamesema klabu itaanza rasmi mazoezi siku ya Jumatano baada ya sikukuu ya Eid kumalizika.

Hajji Manara “Mazoezi rasmi ya Simba yataanza siku ya Jumatano baada ya hizi sikukuu kuisha, pia tunasubiri muongozo wa serikali ili watupe maelekezo yanini vitu gani kufanya na kuzingatia katika kipindi hiki.”

Kumrudisha nchini Kagere au Chama?

Mtendaji mkuu wa Simba alikiri kuumizwa kichwa kwa kuwakosa wachezaji wake wanne waliopo nje ya nchi baada ya serikali kutangaza Ligi kuu kuruhusiwa kerejea kuanzia June Mosi. Wachezaji wa Simba waliopo nje ya nchi ni Meddie Kagere (Rwanda), Sharaff Shiboub (Sudan), Francis Kahata (Kenya) na Clatous Chama (Zambia).

Senzo Masingisa ” Kuna mchezaji mmoja siku ya Jumatatu atawasili nchini ili kuweza kuungana na wenzake kambini, hatuwezi kusema ni mchezaji gani lakini kuna mmoja atakuja siku hiyo. Kama klabu tunafanya mipango yetu lakini hatuwezi kusema kila kitu. Hata hao wengine pia tunaangalia uwezekano wa kua nao.”

Meddie Kagere akiwa na tuzo yake ya ufungaji bora ya msimu wa 2018/2019 aliyopewa na tovuti ya Kandanda.

Usajili.

Mtendaji Mkuu Senzo Masingisa hakusita kugusia swala la usajili huku akisema anaona maneno mitandaoni na pia maoni ya mashabiki katika hilo.

“Kuhusu usajili muda haujafika kwasasa tunajikita katika kumalizia Ligi kwa michezo iliyobaki. Lakini kuna wachezaji wetu ambao tutawabakisha  tayari kuna wachezaji tupo tunamalizana nao kama watatu mambo yakiwa tayari tutawatangazia.

Mlinzi wa Coastal Union anewaniwa kusajiliwa na klabu ya Simba sc.

Lakini kwa wachezaji ambao tutakaowasajili nawahakikishia watakua ni wachezaji wakubwa subirini muda ufike kila kitu kitawekwa wazi mnaona.” Senzo Masingisa.

 

Sambaza....