Ligi

Sababu kwanini YANGA wataifunga SIMBA

Sambaza....

Leo ndiyo tarehe nne mwezi wa kwanza mwaka 2020, tarehe ambayo wengi walikuwa wanaisubiri kwa hamu kwa sababu ya mechi kati ya Simba na Yanga itakayochezwa katika uwanja wa Taifa Dar -es- Salaam , zifuatazo ni sababu ambazo kwanini Yanga wanaweza kuifunga Simba Leo.

KUJIAMINI SANA KWA SIMBA

Simba inajiamini sana kwenye hii mechi , inajiamini wao ni timu bora zaidi kuizidi Yanga na wanaamini wanaweza wakashinda idadi yoyote ya magoli dhidi ya Yanga, inawezekana Simba ni timu bora kwa sasa lakini ukweli ni kwamba kujiamini kupitiliza kunaweza kukufanya usifanye vizuri kwa sababu unaweza ukajikuta unafanya makosa ambayo hukutarajia kuyafanya ndani ya uwanja kwa sababu tu ulijiamini kupitiliza na mpinzani wako akakuadhibu kupitia makosa ambayo umeyafanya.

YANGA KUWA UNDER-DOG

Moja ya faida ambayo Yanga wanayo Leo ni wao kuwa Under-DOG kwenye hii mechi. Kuwa under-dog kuna faida kubwa Sana. Kwanza kunamfanya umpe heshima mpinzani wako , pili unakuwa unacheza kwenye presha ambayo ni ndogo sana , unapocheza kwenye presha ndogo kunakufanya ufanye maamuzi sahihi ndani ya uwanja. Maamuzi ambayo yanakuwa na faida kwenye timu kwa sababu ya umakini wake.

PRESHA KUBWA YA MASHABIKI WA SIMBA

Ukitazama Kati ya mashabiki wa Yanga na Simba , Mashabiki wa Simba wanaonekana kuwa na presha kubwa ya kuilazimisha timu ipate matokeo ndani ya uwanja. Wanaamini wao ni timu bora kuzidi Yanga , wanaamini wanauwezo wa kuifunga Yanga idadi yoyote ya magoli. Kitu hiki kitawapa presha kubwa wachezaji wa Simba , presha ambayo inaweza ikawafanya wajikute wanafanya maamuzi yasiyo sahihi ndani ya uwanja , maamuzi ambayo yanaweza yakawagharimu kutokana na wao kukubali kuivaa hiyo presha , kitu pekee ambacho wanatakiwa kukubaliana nacho ni wao kutoruhusu presha iwavae kwenye mechi ya Leo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.