Ligi Kuu

Sadala Lipangile: KMC haishuki daraja.

Sambaza....

Baada ya matokeo mabovu na yasiyoridhisha wanayoyapata “Kino Boys”   yanayowafanya kushika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara mlinzi Sadala amewahakikishia wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kua timu hiyo haitoshuka daraja.

Sadala amefanya mazungumzo mafupi na tovuti ya Kandanda baada ya kupokea zawadi yake ya Galacha wa mabao inayodhaminiwa na Mgahawa Cafe and Restaurant na kutoa ahadi hiyo kwa mashabiki wa KMC.

Sadala Lipangile akikabidhiwa zawadi yake na afisa masoko wa tovuti Thomas Mselemu baada ya kuibuka galacha wa mabao kwa mwezi January.

 

Sadala ” Kikubwa ninachoweza kusema kwa ushirikiano wa wachezaji pamoja na benchi letu la ufundi tutapambana kwa kila namna uwanjani  ili timu iwe kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo. Tunaumia kukaa huku tulipo kwakweli hatufurahishwi kabisa na matokeo haya.

Sadalla pia hakusita kuwaita mashabiki wa KMC uwanjani ili kuendelea kuwapa nguvu “Wasikate tamaa  kabisa, waje kuiunga mkono timu yao maana wao ndo kila kitu kwetu, bila wao tutazidi kupingukiwa na morali. Wajee waone tunavyoipambania timu yao uwanjani.”

Wachezaji wa KMC wakiwa mazoezini katika uwanja wa Bora Kijitonyama.

Kmc imezidi kua katika hali mbaya katika msimamo baada ya kupokea kichapo cha mabal mawili kwa bila kutoka kwa Simba sc katika mchezo uliopigwa jana usiku.

Mpaka sasa KMC inashika nafasi ya 19 ikiwa imecheza michezo 24 ikiwa na alama 21. Mchezo unaofwata katika VPL ni KMC dhidi ya Simba katika uwanja wa Taifa


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.