Sportpesa

Sevilla: Tunakuja Tanzania

Sambaza....

Klabu ya soka ya nchini Uhispania ya Sevilla fc inayocheza ligi ya Laliga imethibitisha itakuja nchini mwezi May mwaka huu kucheza michezo ya kirafiki na klabu za Tanzania.

Katika ukurasa wao rasmi wa Twitter wameandika “Tutamaliza msimu na mchezo wa kirafiki Tanzania”

Sevilla wanatarajiwa kuja nchini kucheza michezo ya kirafiki na klabu kubwa nchini na Africa Mashariki na Kati kwa ujumla Simba sc na Yanga. Huku safari hiyo ikihisaniwa na Sportpesa ambao ndio wadhamini wakuu wa klabu za Simba na Yanga.

Sevilla ina nyota kama Ben Yeder, Jesus Navas na Ever Banega wanaotamba Laliga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.