Blog

Sichezi kuwafurahisha mashabiki – Molinga

Sambaza....

Kumekuwa na maneno mengi sana kuhusu kiwango cha Mshambuliaji wa Yanga kutoka nchini Congo, David Molinga maarufu kwa jina la Falcao.

Mshambuliaji huyo wakati anakuja Tanzania, WanaYanga walikuwa wana imani naye lakini baada ya kuanza kucheza mechi mbalimbali imani ikaanza kupungua taratibu.

Katika ziara ya mechi za kirafiki zilizochezwa Mwanza , Molinga “Falcao” amefanikiwa kufunga magoli 3 katika mechi mbili alizocheza, goli lake la kwanza alilifunga dhidi ya Pamba fc na jana amefanikiwa kufunga magoli mawili dhidi ya Toto Afrika katika mchezo ambao Yanga wamefunga goli 3-0.

Baada ya mchezo huo kumalizika Molinga alisema kuwa yeye hayupo kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki bali kazi yake kuu kama mshambuliaji ni kufunga na kuisaidia timu yake kufanya vizuri zaidi.

“Nilichelewa kuja , nikawa nahangaika kuzoeana na wenzangu, kwa sasa nazoea na siko kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki “.

Alipoulizwa suala la kupungua uzito na kuaminiwa na kocha, Molinga amedai kuwa anamshukuru sana kocha Mwinyi Zahera.

“Namshukuru sana Mwinyi Zahera ananipa nafasi ya kucheza kila siku na kunipa hali ya kujiamini “. alimalizia mchezaji huyo ambaye hajui kiswahili vizuri.

Yanga itakutana na Zesco United ya Zambia katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya Mabingwa Barani Afrika. Mchezo huo utachezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 14 katika uwanja wa Taifa jijini Dar e salaam kabla ya kurudiana tarehe 27 mwezi huu nchini Zambia.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.