Blog

Simba inarudi tena na ile saa saba mchana ya usajili.

Sambaza....

Unakumbuka kipindi cha usajili jinsi ambavyo Klabu ya Simba ilivyokua inatambulisha wachezaji wake kila ifikapo mida ya saa saba mchana? Basii ulee mtindo unarudi tena kuanzia Jumamosi hii ya tarehe 23 mwezi huu.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ya Twitter na Instagram klabu ya Simba imetangaza kuanza kwa historia mpya kwa klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi. Katika kurasa hizo wameandika “Historia mpya klabu”.

Baada ya maneno hayo mashabiki wamekua wakitaka mufahamu ni nini haswa klabu yao inataka kufanya.

Je Simba inaanza kutangaza usajili mpya? Ama wanatangaza udhamini mpya? Au ni kuuza wachezaji nje ya nchi?

Muda utaongea tusubiri tuone.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.