Ligi Kuu

Simba kapotea njia lazima adhibitiwe Kirumba

Sambaza....

Leo kutakuwepo na mchezo wa ligi kuu kati ya Simba na Alliance ya Mwanza katika uwanja wa CCM kirumba.

Akizungumza na mtandao huu msemaji wa Alliance Jackson Mwafulango amedai kuwa Simba kesho lazima auliwe kwa sababu amepotea njia.

Jackson Mwafulango amedai kuwa walienda kuweka kambi Kenya kwa ajili ya kuwaua Simba na Simba wanatakiwa kujiandaa kwenye hilo.

“Tumeenda Kenya kwa ajili ya kuweka kambi bora na nzuri kwa ajili ya kuwaua Simba hivo wanatakiwa wajiandae vizuri”.

Akizungumza kuhusu timu yake kufanya vibaya kwenye uwanja wa CCM kirumba ukilinganisha na uwanja wa Nyamagana amedai kuwa wamejifunza.

” Tumejifunza na tunataka kuwaonesha Simba kwa sasa  uwanja huu na tutafanya vizuri kwenye mechi hii inabidi wajiandae”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.