Wachezaji wa Simba Pape Sakho na Clatous Chama wakishangilia moja ya magoli yao katika mchezo dhidi ya Horoya.
Mabingwa Afrika

Simba kuanza safari ya Morocco kwa mafungu

Sambaza....

Kikosi cha Simba leo kitaondoka na kuelekea nchini Morocco katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca kukamilisha ratiba ya kundi C.

Wachezaji wa Simba leo wamefanya mazoezi ya mwisho asubuhi hii katika uwanja wao Mo Arena Bunju na baadae alasiri watasafiri kwenda nchini Morocco tayari kwa mchezo utakaopigwa Marchi 31 saa nne usiku wakati huku kwetu itakua ni April mosi saa saba usiku.

“Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho asubuhi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Kikosi kinaondoka nchini saa 9 Alasiri kuelekea Morocco tayari kwa mchezo huo ambao utakuwa wa mwisho wa hatua ya makundi,” taarifa kutoka tovuti ya klabu ilisema.

Kikosi hicho cha Simba ambacho tayari kimeshafuzu kitaondoka na wachezaji 13 pekee pamoja na benchi la ufundi huku wachezaji waliopo timu ya Taifa wataungana na wenzao baadae.

Mzamiru Yasin (katikati) akiwatambuka wachezaji wa Raja Casablanca.

“Kikosi kitaondoka na wachezaji 13 pamoja na benchi la ufundi huku wale ambao wapo kwenye majukumu ya timu za taifa wataungana moja kwa moja na timu ikiwa Morocco,” iliongeza taarifa hiyo.

Mpaka sasa Simba wana alama tisa nafasi ya pili wakati wapinzani wao Raja wapo kileleni wakiwa na alama 13  hivyo matokeo yoyote hayatobadilisha msimamo wa kundi D.

Sambaza....