Stori

Simba kufuru, yabeba mamilioni ya M-bet

Sambaza....

Simba imeingia mkataba na M-bet kwa miaka mitano ambao ulitangazwa July 14 na leo August 8 mkataba huu umetolewa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa habari.

Klabu ya Simba itapata kiasi cha Bil 26 na zaidi katika kipindi cha miaka mitano ya udhamini wao kutoka kampuni ya M-bet!

Thamani ya mkataba wa Simba na wadhamini wao M-bet kwa miaka mitano.

Ahmed Ally akiuzingumzia uhusiano huo mpya wa Simba na M-bet amesema ni matunda ya uwekezaji katika klabu hiyo.

“Ni mkataba mnono zaidi kwa ngazi ya klabu kuwahi kutoea hapa nchini kutokana na mafanikio na uwekezaji mkubwa Simba walioufanya.” Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba

Pia Barbar amesema wameingia mkataba na timu kubwa kwasababu wao ni wakubwa pia nq ni mkataba wa timu kubwa pekee, haihusishi timu ya wanawake wala vijana.

“Simba ni wakubwa na ni lazima ifanye kazi na wakubwa wengine, M-bet ndio kampuni kubwa nchini na ndio inafanya vyema katika industry yao na ndio maana Simba wameamua kuungana nao.” Barbar Gonzales mtendaji mkuu wa klabu ya Simba

“Mkataba huu umelenga 100% kwa timu kubwa pekee na si kwa timu ya Wanawake walaa timu za vijana, na ni kwa mara ya kwanza Tanzania timu inapata mkataba mkubwa kama huu.,” alimalizia Barbar Gonzales

Pia meneja wa masoko wa M-bet ametanabaisha ni kwanini wamechagua kufanya kazi na Simba

“M bet ni kampuni kubwa ya kubashiri hapa nchini na ndio maana tunashirikiana na klabu kubea pia hapa nchini ambayo ni moja tu Simba.” Allen Mushi meneja masoko wa M-bet Tanzania


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.