Ligi Kuu

Simba kuwa na uwanja wiki mbili zijazo

Sambaza....

Maendeleo ya uwanja wa Bunju yamefikia sehemu nzuri. Sehemu ambayo inawapa nafasi Simba kuwa na uwanja wao wa mazoezi baada ya wiki mbili zijazo.

Hayo yamethibitishwa na mkuregenzi mtendaji wa Simba , bwana Crescentius Magori.

“Naomba niwape UPDATES za BUNJU baada ya Wiki 2 Uwanja wa Mazoezi utakuwa Tayari baada ya TAKUKURU kuziachia NYASI hizo baada ya Kukamilika kwa Uchunguzi wa Kesi ya Msingi”-CEO Crescentius Magori

Kwa maana hiyo Simba itakuwa imepiga hatua nyingine kubwa ya kimaendeleo baada ya kupata uwanja wao wa mazoezi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.