Mabingwa Afrika

Simba: Tunafuzu kwenda robo bila mashabiki kuingia bure.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba kupitia msemaji wake Ahmed Ally wamesema wapo tayari kwa mchezo dhidi ya Horoya na wanaitaka robo fainali kwelikweli.

Ahmed Ally amesema akili na nguvu zao wameziwekeza katika mchezo huo na pia wanashukuru mchezo wakuwapelekea robo fainali utapigwa nyumbani.

 

“Akili na nguvu zetu tunakwenda kuziweka Jumamosi ili tuweze kushinda na kufuzu Robo Fainali. Ni mechi yenye namna moja pekee tu kushinda. Mechi hii inatukumbusha mechi ya Wacongo AS Vita, safari hii tupo na Horoya kutoka Guinea.

“Kila mshabiki wa Simba lazima atambue kwamba tutaingia Uwanja wa Mkapa kwenda kupambana kuingia Robo Fainali. Hatuko tayari kuishia kwenye hatua ya makundi na wakati mechi ya kutupeleka robo tutachezea Uwanja wa nyumbani,” Ahmed Ally

Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba Sc

Aidha pia Ahmed amesema wao hawawezi kuweka kiingilio bure katika mchezo huo kama ambavyo Mamelody Sundowns walifanya dhidi ya Al Ahly. Amesema Simba ina mashabiki wengi lakini pia wamewahi kuujaza uwanja huo mara kadha katika michuano hiyo.

“Mamelodi haina mashabiki ni timu ngeni Afrika Kusini hiyo haiwezi kufanywa na Kaizer au Orlando sababu wana mashabiki wa kutosha,” alisema Ahmed Ally

 

Sambaza....