Ligi

Simba wana POINT’S (6 ) zetu lazima wafe tarehe 4 – NUGGAZ

Sambaza....

 

Kuelekea homa ya pambano la watani wa jadi nchini Simba na Yanga litakalochezwa tarehe 4 mwezi wa kwanza mwaka 2020 , Afisa Mhamasishaji wa Yanga amedai kuwa tarehe 4 lazima Simba wafe.

“Kwa sasa timu iko Mbeya inajiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City , tunachoangalia ni sisi kuchukua alama hizo tatu dhidi ya Mbeya City Baada ya hapo tuwatazame Prisons ambao tutacheza nao tarehe 27 mwezi huu”.

“Baada ya sisi kuchukua alama 6 za Mbeya tutakuja Uhuru Stadium kuchukua alama tatu dhidi ya Biashara United , tukimaliza kukusanya hizo alama 9 basi tutaenda kuchukua alama zetu tatu dhidi ya Simba , Simba msimu huu ana alama 6 zetu”.

Kwa sasa acha tumpumulie kwa nyuma hasa tukichukua hizo alama tisa dhidi ya Mbeya City , Prisons na Biashara United na Baada ya hapo basi tutawapita kwa kuchua alama tatu dhidi Yao ” alijinasibu kwa kujiamini Afisa mhamasishaji huyo wa Yanga


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.