Simba Sc
ASFC

Simba wapewa wanajeshi tena, Yanga wapewa kibonde.

Sambaza....

Droo ya hatua ya 64 ya kombe la Azamspirts Federation Cup zimefanyika leo kwenye studio za Azam Media zilizopo Tabata Jijini Dar es salaam.

Yanga ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo wakiifunga Coastal Union msimu uliopita kwa mikwaju ya penalti katika fainali iliyofanyika mkoani Arusha katika Dimba la Sheikh Amri Abeid.

Katika droo hiyi Simba imepangwa kucheza na Eagle FC yenye maskani yake Tabata Dar es salaam ambao ni wanashiriki Ligi ya Mabingwa wa mkoa mchezo utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa upande wa Yanga wao wamepangwa kucheza na Kurugenzi ya Simiyu inayoshiriki First League mchezo utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Michezo hiyo ya Kombe la FA imepangwa kupigwa kati ya December tisa na kumi na moja mwaka huu.

Sambaza....