Ligi Kuu

Simba ya Sven haina mpinzani mikoani !

Sambaza....

Mara ya mwisho kucheza na Mtibwa Sugar ilikuwa siku ambayo kulitokea sintofahamu kwenye klabu ya Simba baada ya kufungwa na Mtibwa Sugar kwenye michuano na Mapinduzi na Mohammed Dewji kutaka kujivua nafasi ya uenyekiti wa bodi ya Simba.

Leo hii Simba imemamaliza hasira zake ambazo Mtibwa Sugar alizisababisha , Kwa hasira zisizo kuwa na kipimo Simba wamewafunga Mtibwa Sugar magoli 3-0 kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro.

 

Magoli ya Simba yalifungwa na John Raphael Bocco , Mohammed Hussein pamoja na Hassan Dilunga. Kwa ushindi huu inaonesha Simba ya kocha Sven ni Simba ambayo ina balaa zito kwenye viwanja vya mikoani.

Tangu achukue nafasi ya Patrick Aussems amecheza mechi tatu za ugenini na ameshinda zote huku akifunga magoli 9 kwenye hizo mechi tatu. Alishinda 2-1 dhidi ya Mbao FC , akashinda 4-1 dhidi ya Alliance na Leo kashinda 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.