Uhamisho

Simba yaikomoa Yanga kwa Kichuya!

Sambaza....

Vita ilianza kwa aliyewa kuwa mchezaji wa UD Songo ambaye alikuwa kwenye mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kujiunga nao msimu huu.

Lakini mwisho wa Siku mchezaji huyo alisajiliwa na Simba . Simba walikuja na dau la milioni 110 , dau ambalo Yanga hawakuwa nalo na kusababisha wamkose mchezaji huyo.

Kabla hata dirisha la usajili halijaisha Yanga walikuwa kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili winger Shiza Kichuya , lakini Simba wamekuja na kumsajili.

Simba wamewazidi tena kwa Mara ya pili kwenye dirisha hili dogo la usajili. Kwa miaka ya hivi karibuni Simba imekuwa ikiwazidi Yanga kwenye usajili dakika za mwisho.

Mfano,  Yanga walikuwa kwenye mazungumzo na Chama lakini Simba wakamnasa , Meddie Kagere alikuwa anaelekea Yanga lakini dakika za mwisho Simba wakamnasa


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.