Ligi Kuu

Simba yakanusha kuwatema Zana na Kwasi

Sambaza....

Kuna habari zinaendelea kuenea kwa sasa ambapo klabu ya Simba inahusishwa kuachana na baadhi ya wachezaji wa kimataifa kama Asante Kwasi, Zana Coulibay na Jurko Murshid.

Habari hizo zinadai kuwa bodi ya Simba ilikaa chini kupitia ripoti ya mwalimu wa Simba ambaye alipendekeza kuachana na Haruna Niyonzima, Zana Coulibaly, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi, James Kotei na Jurko Murshid.

Zana (Kushoto)

Lakini bodi hiyo ikaamua kuwaacha Jurko Murshid, Asante Kwasi na Zana Coulibaly kwa mujibu wa taarifa hizo. Tulipomtafuta Mtendaji mkuu wa Simba alikana hizo taarifa.

“Hizo taarifa ni za uongo, bodi ya Simba haijakaa. Bodi ya Simba ni kitu kikubwa sana kama itakutana basi watu wengi wangejua kuwa imekutana lakini bodi ya ligi haijakutana”- alidai bosi huyo wa Simba


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.