Sambaza....

Said Khamis Ndemla, mara nyingi tumekuwa tukimuona anacheza katika eneo la kiungo mshambuliaji. Lakini katika mechi mbili zilizopita (mechi dhidi ya Stand Unite na mechi dhidi ya Alliance). Said Khamis Ndemla alicheza katika eneo la kiungo wa chini.

Amecheza kama HOLDING MIDFIELDER. Eneo ambalo mara nyingi James Kotei na Jonas Mkude huwa wanalicheza. Lakini kwenye mechi hizi kocha Patrick Aussems ameamua kumwanzisha Said Khamis Ndemla. Eneo hili ndilo eneo ambalo Said Khamis Ndemla alikuwa anacheza awali kabla hajaanza kucheza eneo la kiungo mshambuliaji.

Upi utofauti unaoonekana kwenye timu ya Simba kama Said Khamis Ndemla akicheza eneo la HOLDING MIDFIELDER na Jonas Mkude/James Kotei wakicheza eneo hilo?

MIJONGEO/MOVEMENTS.

Hili ndilo eneo ambalo Linawatofautisha Said Khamis Ndemla na Jonas Mkude pamoja na James Kotei.

Said Khamis Ndemla amekua akianza kutembea kuanzia kwenye eneo lake mpaka eneo la timu pinzani kwa tahadhali zaidi. Hii ni tofauti na kina Jonas Mkude na James Kotei, ambao wao mara nyingi hutumia muda mwingi sana katika eneo lao, ni mara chache sana kwao wao kuwa na tabia ya kwenda kwenye timu pinzani mara nyingi.

MASHUTI MAREFU NA MAFUPI.

Said Khamis Ndemla anauwezo mkubwa wa kupiga mashuti kutoka umbali mrefu ( mfano shuti alilopiga katika mchezo dhidi ya Stand United ,likagonga mwamba na Mohammed Ibrahim akafunga goli ambalo lilikuwa OFFSIDE), hii ni nadra sana kuona katika miguu ya Jonas Mkude na James Kotei. Hata kama wakipiga huwa hayawi na hatari kubwa kama mashuti ya Said Khamis Ndemla.

PASI FUPI FUPI NA NDEFU.

Wote wanauwezo wa kupiga pasi, lakini kuna utofauti katika upigaji wao wa pasi. Kwa mfano, Jonas Mkude mara nyingi anapiga Square passes, ambazo huwa hazina faida kubwa sana kwenye timu. Said Khamis Ndemla huwa anapiga DIRECT PASSES. Ni aina ya wachezaji ambao wanatamani timu iwe mbele tu muda mwingi. Ndiyo maana anapiga Direct Passes sana, na pasi zake nyingi (ziwe ndefu au fupi) zinakuwa za ufasaha na zina madhara. Mfano goli la kwanza kwenye mechi dhidi ya Alliance schools alipiga pasi ndefu ambayo ilisababisha kona iliyozaa goli. Goli la pili alipiga pasi ndefu ambayo ilimkuta Asante Kwasi na kufunga goli.

KUIBA MIPIRA NA KUANZISHA MASHAMBULIZI (TRANSITION).

Kuna wakati timu huwa inashambuliwa, kipindi hiki huitajika mtu ambaye anaweza kuiba mipira na kuanzisha mashambulizi kuelekea timu pinzani (transition). Eneo hili Said Khamis Ndemla yuko vizuri sana kuliko Jonas Mkude pamoja na James Kotei. Na hapo ndipo tunapokuja kuamini kuwa Said Khamis Ndemla ana VISION (kwa sababu anajua mpira Fulani utafika maeneo Fulani ndiyo maana anaiba sana mipira) pia ana ditacte tempo ya mchezo husika.

KUTENGENEZA NAFASI ZA MAGOLI NA KUTOA PASI ZA MWISHO ZA MAGOLI.

Katika mechi dhidi ya Stand United, Said Khamis Ndemla alitengeneza nafasi tatu za magoli yote matatu ambayo Simba waliyafunga katika mechi hiyo. Pia katika mechi dhidi ya Alliance Schools alitoa pasi moja ya mwisho kwa Asante Kwasi. Hivo Said Ndemla huhusika mara nyingi sana katika magoli ya timu kuliko Jonas Mkude pamoja na James Kotei.

GRISI KWENYE MIGUU YA CHAMA.

Tumemuona Chama aking’aa zaidi katika mechi hizi mbili zilizopita (mechi dhidi ya Stand United na Mechi dhidi ya Alliance Schools) ambapo amefunga magoli mawili, na kuhusika sana kwenye magoli mengi ya Simba tofauti na mechi kadhaa hapo nyuma. Hii ni kwa sababu moja tu. Said Khamis Ndemla, hapendi kupiga Square Passes. Hivo mara nyingi Chama huwa anakuwa hana uhaba wa mipira, ndiyo maana humuoni akishuka chini kuchukua mipira kama ambavyo anavyocheza na Jonas Mkude ambaye mara nyingi huwa anapiga square passes ambazo humfanya Chama asiwe anapata mipira mara nyingi na kujikuta akishuka chini mara nyingi kuchukua mipira.

MWISHO.

Timu ambayo ina Said Khamis Ndemla inakuwa na faida moja kuu nayo kuwa na uhakika wa kufunga magoli mengi kwa sababu Said Khamis Ndemla huwa anaamrisha timu iende mbele muda mwingi kwa kupiga pasi maeneo ambayo ni ya hatari tofauti na timu ambayo iko na Jonas Mkude pamoja James Kotei. Kinachokuja kuharibu kwa timu ambayo ina Said Ndemla ni kimoja, haina ugumu wakati wa kujilinda, tofauti na timu ambayo James Kotei yuko ndani.

Sambaza....