EPL

Solskjaer ala kandarasi ya mshahara kiduchu !

Sambaza....

Hatimaye Ole Gunnar Solskjaer apata  mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha Red Devils, Manchester United.

Solskjaer amepewa mkataba wa miaka mitatu baada ya kushinda michezo 14 kati ya 19 aliyoingoza Man U kama kocha wa muda.

Mkataba wa Solskjaer utakuwa unamlipa  paundi milioni 7 kwa msimu ikiwa ni chini ya nusu aliyokuwa akilipwa kocha Jose Mourinho ya paundi milioni 18 kwa msimu.

Usizikose hizi pia…Solskjaer ambaye tayari ameshapendekeza majina ya wachezaji wanaitajika kukisuka kikosi cha Man U na bosi wa klabu hiyo  Ed Woodward amemuhakikishia kutenga fungu  la kutosha kwa usajili pekee, Solskjaer  amepata shavu hilo ambalo kwake yeye lilikuwa kama ndoto aliyokuwa akiiota kila uchao.

Rekodi zake ndani ya klabu hiyo ni nzuri kwani alishawahi kuifungia klabu hiyo magoli 126 katika mechi 366 alizocheza  kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2007.

Pia akiwa kama kocha hadi sasa amesimamia mechi 19, ameshinda 14, sare 2, kupoteza mechi 3, “ cleansheet” michezo 7, asilimia za ushindi ni 74, magoli ya kufunga 40, wastani wa goli 2.11 kwa kila mchezo na kufungwa magoli 17 ikiwa ni wastani wa goli 0.89.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.