Blog

Stars yapanguliwa Mandawa In Ulimwengu Out.

Sambaza....

Kikosi cha timu ya Taifa Tanzania ”Taifa Stars” kinatarajiwa kuondoka leo kuelekea nchini Algeria kucheza mchezo wa kirafiki March 22 dhidi ya wenyeji Algeria na DRC Congo jijini Dar es salaam March 27.

Kikosi hicho kilicho chini ya kocha mkuu Salum Mayanga na msaidizi Hemed Moroco kimefanya mabadiliko ya wachezaji mbalimbali walioitwa awali na kuongeza wengine waliokua hawajaitwa hapo awali.

Wachezaji John Bocco, Thomas Ulimwengu, Farid Mussa na Salim Hamis wameachwa kwa sababu mbalimbali na nafasi zao kuchukuliwa na Rashid Mandawa (BDF Botswana), Himid Mao na Shabani Idd wa Azamfc.

Ikumbukwe baadhi ya wachezaji walitajwa mwanzoni kwenye kikosi hicho na kufanya mashabiki kua na mtazamo tofauti juu ya uteuzi wao haswa Thomas Ulimwengu aliepo nchi Bosnia kwa sasa. Huku wengi wakihoji kuachwa kwa baadhi ya wachezaji haswa Jonas Mkude na Rashidi Mandawa mwenye magoli 11 mpaka sasa kwenye ligi ya Botswana.

Kikosi kamili cha Taifa Stars hiki hapa.


Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x