Ligi Kuu

Sven Van den Broeck tulimkataa YANGA akachukuliwa SIMBA – BUMBULI

Sambaza....

Baada ya habari nyingi za Yanga kutaka kumchukua Patrick Aussems kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Leo hii Afisa Habari Wa Yanga Hassan Bumbuli ametoa siri ambayo wengi tulikuwa hatuijui.

Hassan Bumbuli amesema kuwa kocha mpya wa Simba Sven Van Den Broeck alianza kuitaka Yanga lakini Yanga walimkatalia na akaamua kutuma maombi kwenye klabu ya Simba.

“Sven Van Den Broeck alituma maombi ya kazi kwetu Baada ya Mwinyi Zahera kutimuliwa , sisi tulimkataa na tulimpomkataa aliamua kuomba kazi kwenye klabu ya Simba Baada ya sisi kumkataa”. Alisema Afisa Habari huyo wa Yanga. Yanga bado inatafuta kocha mpya ambaye ataziba pengo la Mwinyi Zahera


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.