Ligi Kuu

Coastal Union kabla ya kufungwa na Simba!

Sambaza....

Wagosi wa kaya kabla ya kupoteza mchezo dhidi ya Simba leo walikua katika kiwango kizuri sana katika Ligi Kuu Bara haswa katika dimba la Mkwakwani Tanga.

Coastal Union ilikua imeshinda michezo mitano mfululizo tena wakizifunga timu ngumu katika VPL kama Tanzania Prisons, Kagera Sugar na Azam fc.

Coastal ikiwa chini wa Mwalim wa timu ya Taifa ya Kilimanjaro Heroes Juma Mgunda imeonekana kua tishio kwa vigogo nchini huku mpaka sasa ikiwa inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 30 nyuma ya vinara Simba sc na Azam wanashika nafasi ya pili.

Wachezaji wa Coastal Union

Bakari Nondo, Hassan Kibailo Ayoub Lyanga na Mtenje Albano ni wachezaji walio na umri mdogo lakini wamekua nguzo muhimu katika mafanikio ya Coastal Union huku wakichagizwa na wachezaji wazoefu kama Ayoub Semtawa na Hijja Ungado.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.