Wawa
Ligi Kuu

Tuachane na Mzamiru na Kagere, Wawa ndiye alikuwa nyota wa mchezo

Sambaza kwa marafiki....

Jana uwanja wa Taifa uliweza kuwa uwanja wa vita kati ya Simba na Azam FC. Vita ambayo ilihusisha jeshi kutoka Kariakoo na jeshi kutoka Chamazi , na mwisho wa siku jeshi kutoka Kariakoo lilifanikiwa kushinda hiyo vita.

Ushindi wa jana wa Simba umeifanya kufikisha alama 15 na kuendelea kujikita kileleni ikiwa imeshinda mechi zote tano ambazo amecheza. Hii ni nafasi nzuri kwa Simba kuendelea kutetea ubingwa wake. Katika mechi hiyo wachezaji wengi walicheza vizuri sana , lakini beki wa Simba , Pascal Wawa anabaki kuwa mchezaji bora kutokana na yeye kuwa imara maeneo yafuatayo.

UWEZO WA KUINGILIA MIPIRA.

Pascal Wawa mara nyingi amekuwa hachezi rafu sana kutokana na yeye kutosubiria mpira umfikie mchezaji wa timu pinzani , yeye husoma uelekeo wa mpira na yeye kuingilia mchezo haraka kabla ya mpira kumfikia mchezaji wa timu pinzani. Hiki alikifanya vizuri kwenye mchezo wa jana , alikuwa ana uwezo wa kusoma uelekeo wa mpira na kuuwahi kabla haujamfikia mshambuliaji wa Azam FC.

UWEZO WA KUCHEZA MIPIRA YA JUU.

Mara zote hii imekuwa silaha yake pia, pamoja na umbo lake kuwa fupi lakini amekuwa na uwezo wa kucheza mipira ya juu. Washambuliaji wa Azam walikuwa warefu lakini yeye alikuwa na uwezo wa kucheza vizuri mipira ya juu .

UWEZO WA KUANZISHA MASHAMBULIZI

Moja ya silaha kubwa ya Simba ya Patrick Aussems ni kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma , na Pascal Wawa amekuwa silaha ya mfumo wa Patrick Aussems kwa kuanzisha mashambulizi vizuri kutoka nyuma.

UWEZO WA KUPIGA PASI NDEFU NA FUPI

Hii jana ilikuwa silaha yake kubwa sana Pascal Wawa ambapo alikuwa anapiga Pasi ndefu na fupi kutoka eneo la Simba kwenda eneo la Azam FC

KUZIBA UWAZI PEMBENI MWA UWANJA

Mara nyingi beki wa kulia wa Simba jana alipokuwa anapanda kushambulia , nyuma kulikuwa kunabaki uwazi. Uwazi ambao Pascal Wawa alikuwa anafanya haraka kuuziba vizuri.

Kwa hiyo haya ni maeneo muhimu ambayo Pascal Wawa aliyatimiza vizuri jana na kumfanya aonekane kama ni nyota wa mchezo wa jana.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.