Blog

Tuache ‘ushamba’, kiatu hakiwezi kuwa gumzo!

Sambaza kwa marafiki....

Kati ya vitu ambavyo vinatufelisha sisi Watanzania ni kupenda kujadili vitu rahisi tukiacha mambo s magumu. Tunajadili vitu vyepesi kwanzia kwenye uchumi, siasa, utalii, michezo, biashara, sanaa, utawala bora, kilimo,haki na sekta nyingine zote. Yes, we deal with petty issue rather than anything else!

Simba Sports Club ni klabu iliyoanzishwa mwaka 1936, imechukua Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania (TPL) mara 20 (hayo ndiyo mashindano makubwa nchini) achana na FA, na mashindano mengine kama Mapinduzi Cup!

Kiatu (kushoto) alichopewa Adam Salamba

Katika nyanja za Kimataifa, Simba Sports Club imefanikiwa kubeba Kagame Cup (mashindano ambayo hata FIFA hawayatambui) na imefika hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Barani Afrika msimu wa 2018/2019, kiujumla Simba Sports Club bado haina mafanikio ya kutisha (tukiweka ushabiki pembeni), nje na ndani ya uwanja. Haina mafanikio ya kutisha kulingana na jina lake lilivyo kubwa nje ya uwanja. Vivyo vivyo kwa Young Africans Club (Yanga) ambayo imeanzishwa mwaka 1935, mafanikio makubwa ya Yanga ni kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania mara 27 achana na mashindano mengine kama nilivyoeleza hapo juu. Hivyo timu zote hizi mbili kongwe hapa nchini, bado hazina mafanikio ya kutisha kulinganisha na majina yake yanavyosikika.

Adam Salamba

Tangu nimezaliwa sijawahi kusikia vilabu hivi viwili vikitaja ama vikitoa taarifa ya mapato na matumizi (Financial Statements) kwa mwaka wowote ule kwa mashabiki na wanachama wake. Huwezi kusikia Simba mwisho mwa msimu wakisema waliuza jezi ngapi na walipata kiasi gani cha shillingi, huwezi kusika Simba wakisema waliuza haki za matangazo kwa vituo gani na walipata Shillingi ngapi, huwezi kusikia Simba wakisema walivuna kiasi gani kutokana na mapato ya mlangoni. Vivyo hivyo kwa watani zao Yanga huwezi kusikia habari hizo, unachoweza kufikia kutoka kwa Simba na Yanga ni kuomba zichangiwe tu!

Na sisi mashibiki na wapenzi wa vilabu hivi tulivyo mazuzu na washamba tunavyopenda kujadili “petty issues” hutokuja kusikia tunahoja mapato na matumizi ya hivi vilabu kwasababu tumezoa kujadili vitu vyepesi. Sisi ni Mabingwa wa kupachikana majina ya hovyo hovyo tu na kuzodoana kusiko na mipaka!

Ever Banega

Ukifanya ulinganisho kati ya hivi vilabu viwili (Simba na Yanga) dhidi ya Sevilla Football Club iliyoanzishwa 25 Januari 1890, Klabu ambayo ipo hapa nchini kwa ziara maalum, utaona kuwa Sevilla FC imeziacha mbali sana hizi timu zetu kubwa hapa nyumbani, hivyo sisi tuna ya kujifunza, kwanzia makocha wetu, viongozi wa timu zetu, wachezaji na sisi mashabiki.

Nimestaajabu kuona mjadala wa mchezaji wa Simba Sports Club, Adam Salamba kuomba viatu vya nyota wa Sevilla Ever Bernega. Bado nimshikwa na bumbuwazi juu ya mjadala huo, na wanaonistaajabisha ni wale wanaomcheka Salamba kwa kuomba viatu vya Banega, wengine wamefika mbali na kusema eti Ever Banega ni mchezaji wa kawaida! Really? Hivi kwa wanaofuatilia mpira wa Ulaya kweli Banega ni wa kawaida? Let’s us be serious… Hivi huu ni ushamba wa kiwango gani?

Ever Banega na Messi wakiwa Timu ya taifa, Argentina

Adam Salamba ndiyo kwanza yupo Simba Sports Club baada ya kutoka Lipuli FC kukutana na mtu kama Ever Banega kwake ni historia kubwa na lazima awe na kumbuka murua kama mchezaji. Utofauti wa Barnega upo kama mbingu na ardhi, Barnega anacheza moja ya Ligi Kuu bora Ulaya na Duniani kwa ujumla, sasa unatakaje Salamba ambaye anacheza Ligi ambayo ni kituko kama kichekesho asiombe kiatu kama kumbukumbu kwake? Salamba anacheza Ligi ambayo haina mdhamini, Ligi ambayo haina mipira wa kuwapa wachezaji waliopachika mabao matatu ‘hat-trick’, unataka akutane na Banega asiondoke hata na kiatu?

Mohammed Hussein akiwa katika uzi wa Ever Banega

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, Ever Banega raia wa Argentina ana utajiri wa kiasi cha $ 19m (Dola millioni 19) sawa na Shillingi billioni 45,600,000,000! Hivi Salamba ana utajiri kiasi gani? Nadhani mpaka sasa amepanga na anamiliki IST kama siyo Harrier ama Crown! (Ana Crown).

Ever Banega anacheza klabu iliyobeba UEFA Europa League mara 5 na yeye akishiriki kuleta makombe hayo, Salamba klabu yake imewahi kubeba hata CAF Confederation Cup? Sasa kwanini tumcheke? Ever Banega anacheza klabu yenye uwanja wake unaobeba mashabiki 43,893 (Ramon Sanchez Pjizan), sasa Salamba klabu yake ina hata uwanja wa mazoezi Gym? kama siyo, Kwanini tunamcheka Adam

Wachezaji wa Simba mara baada ya mchezo kumalizika

Kitendo cha wachezaji kubadilishana ama kuombana jezi, viatu ni cha kawaida kwani husaidia kuweka kumbukumbu maishani mwao. Leo Messi, Cristiano Ronaldo, Steven Gerrard, Wayne Rooney, Zlatan Ibrahimovic, Andrea Pirlo, Neymar Jr na nyota kibao huwa wanafanya na wameshawahi kufanya, kwanini tuona kwa Adam Salamba ni ajabu?

Kwa wanaosema Ever Banega ni mchezaji wa kawaida, wajue tu kuwa Leo Messi ana jezi ya Lanzine sasa sijui Barnega na Lanzini nani ni mchezaji maarufu na mkubwa! Tuache ushamba Watanzania, common sense is not so common. Hata viatu navyo ni gumzo?


Imeaandaliwa na, Sebastian Emmanuel
Media and Political Consultant.
Mafinga, Iringa, Tanzania.
0745 393 236

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.