Yanga mazoezini
Ligi Kuu

U-Underdog wa Yanga ukitumika vizuri, Simba anakufa.

Sambaza kwa marafiki....

U-Underdog wa Yanga ukitumika vizuri, Simba anakufa.

Inawezekana kwa sasa imani imepungua sana kwenye timu ya Yanga baada ya Sinba kuonekana kwenye mechi dhidi ya Al Alhly  kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika.

Mechi ilionesha ubora wa Simba. Walifanikiwa kuwatawala Al Alhly kwa kiasi kikubwa. Kitu ambacho kimewaongezea hari kubwa kuelekea kwenye mechi ya Leo.

Kwa matokeo hayo ambayo Simba wameyapata dhidi ya timu kubwa barani Afrika yamezalisha vitu viwili kuelekea kwenye hii mechi.

Kitu cha kwanza ni kuongeza hari kubwa ndani ya kikosi cha Simba. Hari ambayo imeongeza kujiamini sana kwa Simba kuelekea kwenye mechi hii ya Leo.

Kuna madhara sana ya kujiamini sana , kwa sababu timu inakuwa na presha kubwa kwa sababu inakuwa imejiaminisha kuwa inashinda.

Ukijiaminisha unashinda mechi husika, kila sekunde lazima ujawe na presha ya kutafuta matokeo ya ushindi.

Na kwa bahati mbaya unapokuwa na presha kubwa ndani yako na dakika zikawa zinaenda bila kupata matokeo ya ushindi lazima u-panic .

Na ndipo hapo unakuwa unafanya makosa mengi ya kinidhamu ndani ya mchezo, makosa ambayo yanaweza kukuadhibu.

Kisaikolojia hapa panaweza kuwa na msaada kwa Yanga, ila watapata msaada zaidi watakapokuwa na mwendelezo wa ukimya wao.

Wamekaa kimya sana, kwa kifupi Yanga wamekuwa wanyonge sana kuelekea mchezo wa Leo. Wanyonge haswaaa.

Hapa ndipo ninapopata nguvu ya kuamini kuwa Yanga katika mchezo wa leo watafanya vizuri tofauti na wengi wanavyotazama.

Kwanini nasema hivo ?, kama nilivyokuambia hapo juu Yanga katika mchezo wa leo wanaingia wakiwa wanyonge sana.

Hii ina maana gani ?, Yanga wamekubali kuwa wao ni wadogo kwenye hii mechi yani ni Under-Dogs. Hii itakuwa na faida kubwa sana kwao.

Kukubali kuwa ni wadogo kwenye hii mechi kutawafanya wacheze wakiwa wanajiamini kawaida. Wakicheza kwa kujiamini kawaida watakuwa na umakini mkubwa ndani yao.

Umakini unapokuwa ndani ya wachezaji kunakuwa na nidhamu kubwa ya wachezaji wanapokuwa na mpira na wanapokuwa hawana mpira.

Nidhamu hii itawafanya Yanga kuwa makini kila wanapokuwa na mpira kwa kuhakikisha kila mpira wanaopata wautumie kwa faida kubwa.

Na nidhamu hii itawafanya wawe makini kila wanapokuwa hawana mpira. Na hii itawapa nafasi kubwa sana kuwa na uhakika na wanachokifanya.

Kwa kifupi hawatoingia kwa kupania kwa sababu ya wao kuingia kwa kukubali ni wadogo kwenye hii mechi.

Presha inakuwa ndogo sana ndani yao, presha inapokuwa ndogo ndani yao wanakuwa na uhakika wa kuepukana na makosa mengi binafsi.

Hivo watawalazimisha Simba wajiamini sana, wakijiamini sana kuna asilimia kubwa ya wao kufanya makosa mengi binafsi, ambayo Yanga wanatakiwa kuyatumia kuwaadhibu.

Kwa hiyo Kisaikolojia Yanga tayari wameshajitengenezea mazingira mazuri ya wao kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa Leo.

Simba wataingia kumiliki mpira na Yanga wataingia kwa ajili ya kuzuia kwenye hii mechi. Hii itachangizwa na aina ya mpira ambao timu hizi hucheza.

Mara nyingi Simba huwa wanamiliki mpira, huwezi kushindana nao kwenye hili. Kwa hiyo Yanga wanatakiwa kukaa nyuma na kuhakikisha wanafanya mashambulizi ya kushtukiza.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.