AFCON

Uganda wataja kikosi chao kuelekea mechi na Tanzania

Sambaza....

Kocha wa Timu ya Taifa ya Uganda “The Cranes” Miluton Sredojevic ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 30 watakaokwenda kuvaana na Tanzania katika michezo ya kufuzu Afcon 2023.

Micho amemrudisha kikosini mlinzi Joseph Ochaya kutoka Arab Contacrots ya Misri na mlinda mlango Salim Magoola kutoka Ricahard Bay ya Afrika Kusini. Ambao mara ya mwisho waliitwa kikosini katika mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya Malawi 2021.

Kikosi kamili cha Uganda “The Cranes”

Uganda wanakwenda kucheza michezo miwili dhidi ya mahasimu wao Tanzania ambapo itawalazimu kucheza michezo yote nje ya kwao Uganda kutokana na kukosa uwanja wenye sifa.

Mchezo wa kwanza utapigwa Misri katika Dimba la Suez Canal Authority Machi 27 kabla yakurudiana tena siku nne mbele katika Dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.


Sambaza....