Tetesi

Ulimwengu atemwa

Sambaza....

Safari yake ni ya kishujaa , toka akiwa TP Mazembe na akafanikiwa kushinda taji la ligi ya mabingwa barani Afrika.

Baada ya kutoka TP Mazembe alienda Sudan kabla hajaenda Algeria kucheza kwenye timu ya Saoura, Saoura ilishiriki michuano ya ligi ya mabingwa na kufika hatua ya makundi.

Ulimwengu akiwa na kikosi cha Soura kilipokuja Tanzania kucheza na Simba Sc, Ligi ya Mabingwa Afrika

Kuna habari za ndani ya klabu hiyo kuwa Thomas Ulimwengu ameachwa na timu hiyo. Tumejaribu kuwatafuta watu wa karibu wa Thomas Ulimwengu lakini hawakupatikana , lakini habari zinazoeenea Algeria kwenye vyombo vya habari ni Thomas Ulimwengu kuachwa na timu hiyo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.