Ligi Kuu

Wachezaji wangu wananiangusha-Kocha wa Simba

Sambaza....

Jana kulichezwa mechi Kali Kati ya Simba na Namungo FC. Kabla ya mechi hiyo Namungo FC walikuwa hawajawahi kupoteza hata mechi moja kwenye mechi tatu za mwisho walizocheza ugenini.

Simba kwa msimu huu hawajawahi kupoteza hata mechi moja walizocheza katika uwanja wa nyumbani. Jana walizidi kuishikiria rekodi yao kwa kuwafunga Namungo FC kwa magoli 3-2.

Ushindi ambao unazidi kuwaweka juu kileleni . Ushindi wa magoli 3-2 , umeifanya Simba iwe imeruhusu magoli 6 kwenye mechi nne zilizopita.

Baada ya mchezo huo kocha wa Simba alisema kuwa hujaridhika na mchezo huo kwa sababu wachezaji wake wanacheza sana pasi za nyuma.

“Wachezaji wanacheza sana pasi za nyuma badala ya kucheza pasi kwenda mbele . Hili ni tatizo na naamini tutalifanyia kazi kwenye mazoezi” alimalizia kocha huyo mkuu wa Simba.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.