Sportpesa

Wafahamu wababe wa Ulaya wanaokuja kuivaa Simba

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya soka ya Sevilla ya nchini Hispania inayoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama Laliga wanatarajia kuja nchini May mwaka huu kukipiga na “Wekundu wa Msimbazi” Simba sc.
Sevilla wanatarajiwa kukipiga na Simba katika dimba la uwanja wa Taifa “Kwa Mkapa” jijini Dar es salaam May 23.

Sevilla mpaka sasa wanashika nafasi ya 6 wakiwa na alama 55 katika Laliga huku bingwa tayari akiwa Barcelona, wakiwa wamebakisha michezo miwili kumalizia ligi.

Klabu ya Sevilla ilianzishwa January 25 mwaka 1890 nchini Hispania ikijulikana kama Sevilla fc huku jina la utani wakijulikana kama “The whites and red.”

Kwa sasa Sevilla wanatumia uwanja wa Ramon Sanchez wenye uwezo wa kubeba watazamaji 43,000. Ikiwa chini ya Rais Josse Castro Carmona.

Mataji ya Sevilla

1. National League – 1

2. Spanish cup 5

3. Spanish Super cup 1

4. Europa Cup 5

5. Uefa super cup 1

 

Kwa sasa Sevilla ipo chini ya mwalimu Joaquin Caparros, wakiwa na nyota mbalimbali wanaowategemea kama Ben Yedder mwenye mabao 17 na nahodha wao Ever Banega. Baadhi ya nyota wengine ni kama Jesus Navas, Roque Messa,  Sarabia na Andre Silva.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.