ASFC

Wananchi wanashuka dimbani kuifwata Simba.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga leo jioni itashuka dimbani katika mchezo wa raundi ya nne ya kombe la FA maarufu kama Azamsports Federation Cup.

Yanga watakua nyumbani wakiwakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi saa moja jioni mchezo unaotarajiwa kuwa wa upinzani wa hali ya juu kutokana na historia zinapokutana timu hizi mbili

 

Tayari watani wa jadi wa Yanga wameshafuzu raundi inayofuata ya michuano hiyo kwa kuwafunga African Sporta kwa mabao manne kwa sifuri. Hivyo Yanga leo nao watashuka dimbani wakitafuta tiketi ya robo fainali mbele ya Wajelajela ambao hawafanyi vyema kwenye ligi kuu.

Wananchi wanaingia dimbani wakiwa mabingwa watetezi wa kombe hilo wakiendeleza ndoto yao yakutaka kubeba makombe yote mawili kama ambavyo walifanya msimu uliomalizikaa walipotwaa Ligi kuu na kombe la FA.

 

Kwa upande wa Prisons wao hawana chakupoteza kwani wamekua wakifanya hovyo katika Ligi na kupelekea kuwa nafasi za chini katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Katika michuano hiyo leo kutakua na mchezo mwingine mmoja ambapo Geita Gold watakua nyumbani Nyankubu kuvaana na Green Worriers kutoka Dar es salaam.

Sambaza....