Sportpesa

Wapinzani wa Simba wamaliza Ligi kibabe

Sambaza....

Wakali kutoka Hispania wanaoshirki Ligi Kuu ya nchini humo maarufu kama Laliga Sevilla fc imemaliza ligi hiyo wakiwa kifua mbele katika uwanja wao wa nyumbani.

Sevilla ambao wanatarajiwa kucheza na Simba May 23 mwaka huu katika dimba la Taifa “Kwa Mkapa” wamemaliza ligi kwa ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Athletico Bilbao .

Mabao ya Ben Yeder na Munir yalitosha kuipa ushindi Sevilla na kuwahakikishia nafasi ya kucheza Europa League msimu ujao.

Kwa ushindi huo sasa Sevilla inamaliza Laliga ikiwa katika nafasi ya 6 ikiwa na alama 59. Bingwa wa Ligi hiyo msimu huu ni Barcelona akifwatiwa na Athletico Madrid na Real Madrid katika nafasi ya pili na tatu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.