Sambaza....

Kwa hali ya kawaida timu ambayo haifungwi au inashinda kwa ushindi finyu sana ikiwa na mchezo mzuri kabisa, unaweza kujua wapi pa kuanza kuangalia na kupamulika zaidi.

Katika michezo 7 ya ligi kuu Lipuli imeshinda mechi moja, sare tano na kupoteza moja. Katika hizi mechi amefunga magoli matatu na kufungwa matatu.

Mchezo huo mmoja ambao Lipuli imeshinda ni katika uwanja wa nyumbani, Samora, dhidi ya timu dhaifu ya Alliance School tena ushindi wa goli moja tu. Mchezo mmoja aliopoteza ni dhidi ya Singida ugenini.

Rekodi ya Lipuli FC

Safu ya ulinzi ipo imara kabisa na bila shaka viungo, lakini kitu ambacho benchi la ufundi inatakiwa kuangalia tatizo la ufungaji mabao. Hili likitatuliwa, timu hii kipenzi cha Wanairinga itafanya vizuri zaidi ya sasa. Sare na ushindi dhaifu zitaibakiza tu Lipuli Ligi kuu lakini sio kugombania taji.

Ushauri wa wazi, Lipuli ibadili mbinu za ushambuliaji au ikubali kuingia sokoni kutafuta mshambuliaji ambae anaweza kusaidiana na waliopo sasa ili ipate matokeo.

Leo pia itakuwa uwanjani kupambana dhidi ya Stand United ambayo sio timu ya lelemama, uongozi wa Lipuli umetoa wito wa mashabiki kujaa uwanjani kuipa sapoti na pia bila shaka kwa lengo pia la kutunisha mfuko wa Lipuli FC.

Sambaza....