Sambaza....

Kocha wa Manchester United Jose Mourihno ndiye kocha ambaye amechaguliwa kwa kura nyingi kuwa kocha wa kwanza kuondoka katika ligi kuu England akifuatiwa na Mark Hughes wa Southampton.

Kocha huyo ambaye ameandikisha matokeo mabovu toka katika michezo ya kujiandaa na msimu amepewa alama 8/11 kuondoka katika kibarua hicho huku Mark Hughes na Neil Warnock wa Cardiff City wakifuatia kwa karibu kwa alama 7/11 kama makocha ambao wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuondoka katika vilabu vyao.

Aidha miongoni mwa makocha ambao wanapewa nafasi kubwa zaidi kuchukua nafasi ya Mourihno kama akiondoka Manchester United ni mchezaji na kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane ambaye amepewa alama 8/11.

Hata hivyo kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte (8/1) na kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger (10/1) pia wanapewa nafasi kubwa ya kukirithi kiti cha Jose Mourihno kunako Manchester United.

Makocha wanaopewa nafasi kubwa kuanza kutimuliwa kwenye EPL:

8/11 Jose Mourinho (Manchester United)

7/1 Mark Hughes (Southampton)

7/1 Neil Warnock (Cardiff City)

10/1 Rafa Benitez (Newcastle United)

12/1 Claude Puel (Leicester City)

14/1 Sean Dyche (Burnley)

Makocha wanaopewa nafasi kubwa kukirithi kiti cha Jose Mourihno:

8/11 Zinedine Zidane

8/1 Antonio Conte

10/1 Arsene Wenger

14/1 Mauricio Pochettino

16/1 Joachim Loew

Sambaza....