Ligi Kuu

Yanga kuanza ilipoishia!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga sc imethibitisha itacheza mchezo wa kirafiki kabla ya kuendelea na ligi ambapo imepangwa kuanza kula kiporo chake dhidi ya Mwadui fc mkoani Shinyanga katika dimba la Kambarage.

Yanga itacheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya KMC “Kino Boys” katika dimba la Uhuru siku ya Jumapili saa kumi jioni huku mchezo huo ukirushwa na kituo cha Azam tv.

Kabla ya Ligi kusimama kutokana na janga la corona Yanga ilicheza mchezo wake wa mwisho wa Ligi dhidi ya KMC na kupoteza kwa bao moja kwa sifuri katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Yanga wamesema watatumia mchezo huo kama tathmini kwa mambo ya ndani na nje ya uwanja. Kwa maana watatumia mchezo huo kutazama utimamu wa kikosi chao lakini pia kuanza kuangalia jinsi ya  kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa corona.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.