Ligi Kuu

YANGA ni kubwa kuliko mchezaji, Ngassa atulie – NUGAZ

Sambaza....

 

Baada ya sakata la Yanga na Mrisho Khalfan Ngassa kupamba moto kwenye mitandao ya kijamii kutokana na Mrisho Khalfan Ngassa kuwadai Yanga shilingi Milioni 15 za kitanzania ambazo ni madai yake ya ada ya uhamisho Leo hii Afisa Mhamasishaji wa Yanga amemjibu Mrisho Ngassa.

“Ni kweli kuna wachezaji wanne wa Yanga wanatudai , kutokana na hali Mbaya ya uchumi tulikuwa tunawalipa kwa awamu. Tulianza na Vincent Andrew Dante tukamlipa, aliyekuwa anafuata ni Mrisho Khalfan Ngassa”.

“Kabla ya Mrisho Khalfan Ngassa kuandika vile kwenye mitandao ya kijamii , nilikuwa nimezungumza naye binafsi lakini cha kushangaza kesho yake akaenda kuandika vile kwenye mitandao ya kijamii, niliumia sana”.

“Nataka kuwaambia wachezaji kuwa hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu, tuliwaambia uongozi huu ulikuta madeni mengi , hivo hela zimekuwa zikilipa madeni watuvumilie tunawalipa kwa awamu na kesho jumanne Mrisho Ngassa atalipwa pesa zake ” alimalizia hivo ndugu Antonio Nugaz


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.