Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa na kocha wa viungo
Shirikisho Afrika

Yanga: Sasa Tunawakilisha Wote si Tanzania Pekee

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants uongozi wa Yanga wameongea na mashababiki wao kupitia kwa Wanahabari za michezo huku wakitaja viingilio pamoja na ratiba ya mchezo huo kiujumla.

Kuelekea mchezo huo msemaji wa Yanga Alli Kamwe amesema “Kuanzia sasa hivi Klabu ya Yanga tunazungumza kwa niaba ya timu zote za nchi hii lakini pia kwa niaba ya Burundi, Rwanda, Congo, Kenya, Sudan na Uganda linapokuja swala la Kimataifa hivyo ni vyema mkatulia kutusikiliza.”

Kuelekea mchezo huo Alli Kamwe ametangaza viingilio vitakavyotumika pamoja na muda wa mchezo utakaochezwa huku ukitoka kuchezeka usiku na sasa utapigwa jioni.

Alli Kamwe.

Alli Kamwe “Mechi itapigwa siku ya Jumatano May 10 jioni katika Uwanja wa Benjamini Mkapa. Tumewapa zawadi ya kiingilio mashabiki wa Yanga hivyo tumeweka viingilio rafiki kabisa kutokana na hadhi ya mchezo wenyewe wa nusu fainali ili kila mtu awepo kiwanjani. 

Viingilio katika mchezo huo vitakua ni VIP A 30,000,  VIP B  20,000, VIP C  10,000 na kule mzunguko kwa wenzangu namimi ni 3,000 ukinunua kabla ya mchezo na siku ya mchezo itakua 5,000.”

Kamwe pia amesema tayari timu ilishaanza safari kutoka Singida huku wakitegemewa kufika Dar es salaam leo ili wapumzike na waweze kuingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Marumo Gallants.

Marumo Gallants

“Tuna kama siku nne tu hivi kuelekea katika mchezo wa nusu fainali, wachezaji watatua leo watapumzika siku moja halafu wataingia kambini kuelekea katika mchezo wa Jumatano,” alimalia Alli Kamwe

Yanga wanatarajiwa kuikaribisha Mallumo Gallants ya Afrika Kusini iliyo chini ya kocha wa zamani wa Simba Dyllan Kerr ambao walitinga hatua hiyo baada ya kuwaondosha matajiri wa Misri Pyramids FC kwa jumla ya mabao mawili kwa moja. 

Sambaza....