Ligi

Yanga vs Prisons kucheza kwenye Uwanja wa NDONDO !

Sambaza....

 

Mchezo kati ya Tanzania Prisons dhidi ya wageni wao Yanga sc umeshindwa kupigwa jijini Mbeya katika dimba la Sokoine kutokana na uwanja kuharibika baada ya shughuli ya kijamii iliyofanyika uwanjani hapo.

Mchezo huo ulikua upigwe kesho Ijumaa katika dimba la Sokoine sasa utapigwa katika dimba la Samora mkoani Iringa siku ya kesho na hii ni baada ya kushindwa kufanyika Sokoine baada ya eneo la kuchezea kuharibika vibaya kutokana na “shoo” ya muziki iliyofanyika uwanjani hapo siku ya tarehe 25 katika sikukui ya Noel.

Mchezo huo umehamishwa huku barua ya bodi ya ligi ikithibitisha hilo. Hivyo sasa timu zote mbili zinajiandaa kusafiri kuelekea mkoani Iringa tayari kwa mchezo huo.

Sasa imekua kama ni neema kwa upande wa mashabiki wa Iringa baada ya kuletewa burudani hiyo ya mchezo mkali na wa kusisimua wa Ligi Kuu Bara.
Ikumbukwe mpaka sasa Prisons ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.