ASFC

Yanga Watinga Nusu Fainali, Mayele Atoa Gundu

Sambaza....

Wananchi wameendeleza rekodi yao nzuri mbele ya Wachimba dhababu Geita Gold baada ya kupata ushindi mwembamba na kufanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Bao pekee la Fiston Kalala Mayele aliyeingia kipindi cha pili lilitosha kuipa ushindi wa bao moja bila mbele ya Geita Gold na kuwafanya Wananchi kuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea kutetea kombe lao. Kwa Fiston Mayele hilo linakua bao lake la kwanza msimu huu katika michuano hiyo.

 

Yanga mabingwa watetezi wa kombe hilo sasa wanakwenda kukutana na Singida Big Stars katika mchezo wa nusu fainali itakayofanyika katika dimba la Liti mkoani Singida.

Kipigo hicho kinakua ni muendelezo wa rekodi nzuri ya Yanga mbele ya Geita Gold kwani msimu huu katika Ligi waliwafunga nje ndani na pia msimu uliopita waliwatoa pia katika michuano ya kombe la FA katika hatua ya robo fainali pia.

Kwa ushindi wa leo kunawafanya Wananchi Yanga kunyemelea makombe yote mawili ya ndani kwani katika Ligi wao ndio vinara na wapo katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao. Pia katika michuano ya Shirikisho wapo robo fainali.

Sambaza....