ASFC

Yanga yaifwata Simba

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi mbele ya Tanzania Prisons katika mchezo wa raundi ya nne wa Kombe la FA maarufu kama Azamsports Federation Cup.

Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo wamepata ushindi wa mabao manne kwa moja katika mchezo uliopigwa katika Dimba la Azam Complex Chamanzi.

 

Yanga ndio walikua wakwanza kupata goli kupitia kwa mlinzi wake wa kati Bakari Mwamnyeto dakika ya 52 kabla ya Jumanne Elfadhili kuwasawazishia Tanzania Prisons dakika ya 60.

Clement Mzize alieingia kipindi cha pili aliipatia Yanga mabao mawili katika dakika ya 70 na 88 kabla ya Aziz Ki kukamilisha kalamu ya mabao kwa kufunga bao la nne kupitia mkwaju wa penati. 

Clement Mzize.

Katika michezo ya awali ya kombe hilo iliyopigwa saa kumi jioni Singida United waliifunga JKT Tanzania bao moja bila, Geita Gold nao waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Green Worries.

Kwa ushindi huo sasa Yanga wanaifwata Simba robo fainali ya michuano hiyo ambayo Yanga ndio bingwa mtetezi wa kombe hilo.

Sambaza....